Monday, July 11, 2011

HASSAN MAAJAR TRUST




Taasisi ya Hassan Maajar Trust kuanzisha kampeni ya kusaidiakutokomeza

uhaba wa madawati mashuleni


   Dar es Salaam Jumatatu, 11 Julai 2011: Mkewa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete, leo hii amezinduataasisi isiyokua ya kiserikali ijulikanayo kamaHassan Maajar Trust (“HMT”), ikiwa na lengo la kusaidia sekta ya elimu nchinikwa kuanzisha kampeni yenye lengo la kukusanya shilingi bilioni 3 katikakipindi cha miaka 2 hadi 3 ijayo. Fedha zitakazochangwa zitatumika kwa ajili yaununuzi wa madawati kwa shule za umma za msingi na sekondari ili kuboreshaelimu nchini.

Kabla ya kuzindua nembo ya taasisi hiyoMama Kikwete alisema kuwa taasisi hiyo imeanzishwa wakati muafaka  kwa sababu “ni wajibu wa kizazi chetu kuhakiksha kwamba haitokei tena watoto wetukukaa sakafuni wawapo madarasni mwao

Akiongea wakati wa Uzinduzi  wa taasisi ya HMT Balozi Mwanaidi Maajar, alisema, "Kampeni itaendeshwa  kwa jina la Dawati kwa kila Mtoto au A Deskfor every child kwa kiingereza, na kampeni hii itafanyika nchiniTanzania na Marekani. Uzinduzi rasmi wa kampeni hii utafanyika tutakapokaribiamwisho  wa mwaka na tarehe ya siku yauzinduzi huo itatangazwa mapema kabla ya siku ya tukio"

Mbali na kampeni hii ya "Dawatikwa kila mtoto",taasisi hii itajihusisha katika miradi mingine yakusaidia vifaa vya shule ili kuboresha elimu na kuendeleza michezo.

Jina la HMT limekuja kwa heshima yaHassan Shariff Maajar, aliyefariki mwaka 2006 kutokana na ajali ya barabaraniiliyotokea huko Mbabane, Swaziland.

HMT imeanzishwa na familia na marafiki waHassan, kama kumbukumbu yake na Hassan alikutwa na umauti akiwa na umri wamiaka 18 huko Mbabane, Swaziland alikokua akisoma katika chuo cha WaterfordKamhlaba United World College.

Hassan alikuwa kijana mmoja hodari,mahiri na mchapakazi  ambaye alikuwa nashauku ya michezo na kutoa kwa ajili ya kusaidia jamii. Hassan alikua mchezajiwa mpira wa kikapu na alikua nahodha wa timu ya shuleni kwake hadi aliokutwa naumauti.

Hassan alipenda kusaidia jamii na mudamwingi alijitolea kufundisha michezo kwenye shule za watoto walemavu huko Mbabane, Swaziland.

Kwa kuutambua moyo huu, familia namarafiki zake tumehamasika kuunda taasisi hii kamakumbukumbu yake.


Takwimu kutoka Wizara ya Elimu naMafunzo ya Ufundi zinaonyesha kuwa shule za msingi na sekondari zina uhaba wamadawati na viti milioni 3.

BaloziMaajar alisema "HMT inaamini kuwa uhaba wa madawatimashuleni una athari kubwa kwa utoaji wa elimu nchini na tunatoa wito wa wadauwote tufanye juhudi zote ili kutatua tatizo hili”


Mwenyekiti alisema zaidi kuwa kunauwekano mkubwa wa kumwezesha kila mtoto nchini kupata dawati na kiti katikakipindi cha miaka miwili hadi mitatu lakini suahal hili linahitaji mshikamanokwa kila mtu kutoka Nyanja tofauti na jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kusaidia kufanikisha jambo hili.

"Tunatarajiakwamba watu kutoka nyanja zote za maisha watajitolea kupitia HMT kuchangia madawati,"alisema Mwenyekiti wakati akiongea na vyombo vya habari.

Katika kampeni hii, HMT itatumia njiambalimbali kukusanya michango, ikiwa ni pamoja na maombi ya moja kwa mojakutoka kwa wananchi na kwa kutumia vyombo vya habari ili kufikisha ujumbekwenye jamii.

Tunahamasisha watu kuchangia chochoteikiwemo nguo, vyombo vya ndani, viatu, vitu ya watoto, vitabu, pia tunaombamakampuni kwa upande mwingine, kuchangia kutoa vitu wanavyotengeneza au hudumawanazotoa.

HMT imefungua duka la hisani pale jengola Arcade, Mikocheni kwa ajili ya kuuza vitu mbalimbali vitakavyotolewa kama mchango ili kulipia gharama za uendeshaji kusudifedha zote zitakazopatikana zitumike kwa ajili ya kununulia madawati.

Bodi ya HMT itaunda kamati yakuchangisha fedha, ambayo itakuwa na jukumu la kutafuta fedha na kuhakikishakwamba fedha zilizokusanywa zinahifadhiwa kwenye akaunti za benki za HMT nakutumika kwa kazi iliyokusudiwa. Kamati pia itakuwa na jukumu la kutoa taarifakwa umma kila mwaka kuonyesha makusanyo na matumizi ikianisha idadi ya madawatiyaliyopatikana.


Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea, www.hassanmaajartrust.org

Au wasiliana na:
Fredrick Felix Njoka,
Public RelationsExecutive,
Aggrey&Clifford,
Tel: +255-772-131367
Email: Fredrick@aggreyclifford.com

 PICHA:: SHUKRAN ANKAL