Saturday, March 20, 2010

MJADALA ::NANI NA LINI TUPAKE HINA

MJADALA ::NANI NA LINI TUPAKE HINA

JAMANI NAOMBENI LEO MNISAIDIE KATIKA HILI...HII HINA AMBAYO MAHARUSI HUPAKWA NI IMEKAA KIDINI ZAIDI AU UTAMADUNI WA BARA FULANI KAMA ASIA TUMEIGA AU NI VP??? MAANA KUNA SIKU NILISKIA KAMA HUJAOLEWA HUNA RUHUSA YA KUPAKA ILEE HINA YA HADI MWILI, UPAKE SUNA TU MKONONI KAMA TUPAKAVYO SIKU ZA EID. CHAKUSHANGAZA...SIKU HIZI NAMKUTA SHOST HANA HARUSI WALA HAJAOLEWA ANAPAKA HINA....UKIULIZA VIPI BIBIE UNAENDA HARUSINI NAAMBIWA WAPIII NAJIANDAAA NIENDE KWENYE RUSHA ROHO MIE. HEBU TUFUNGUANE MACHO NA AKILI...ili tusishangaane NB:: KAMA WAMJUA MPAKA HINA AMBAYE ANAWEZA NIJIBU MASWALI YANGU NIPE CONTACT YAKE....NIKAONGEE NAEEEE PLZZZ


11 comments:

Anonymous said...

Kwakweli kwa upeo wangu mdogo nilo nao najua hina au piko ni sunnah na kwa mazoea ya sisi watu wa bara tunaamini hina au piko kuchora ni mpaka siku yako ya kuolewa au hina mpaka eid hadi eid na pia ni kwa waislamu tu.ila kwa jinsi ninavyoelewa kwa uhalisia kabisa hina au piko ni pambo la mwanamke yoyote na isitoshe kuna aina mbalimbali za michoro ambayo ukienda hata kwa mchoraji anakuwa na upeo akuchore kulingana na shughuli ya ina gani uendayo kama huna shughuli ama harusi basi kuna michoro simple ambayo anaweza kukuchora na mwanamke ukapendeza na kuwa na mvuto mbele ya wanayokutazama na kwa wale mama wa nyumbani kuna michoro amabyo akichora ipo maalum kwa ajili ya kumfurahisha mumewe na pia kuna wasichana ambao huchora tatoo za hina ama piko migongoni,viunoni,mapajani ama hata kifuani ama shingoni kama fasheni ama kujifurahisha nafsi zao nao huwa katika dini na madhehebu mbalimbali na pia kwa mabiharusi nao kuna dizaini ya michoro amabayo inaashiria kabisa mtu huyu kama si bi harusi basi msimamizi kwahiyo kwa upande wangu naamini kila mtu ana uhuru na matashi ya kupaka piko au hina apendavyo mfano kama mimi mara nyingi napenda kupaka piko na hina simple ambapo nip[o kazini lakini michoro amabayo ni simpo lakini inavutia na bila ya kupaka vitu hivyo najisikia nimepunguikiwa na kitu kwa ujumla hina na piko ni hobi au upenzi wa moyoni

ASANTE

FROM BIMAMMY

Anonymous said...

Da Shamim, hinna ni asili ya watu wa pwani.na zamani hadi sasa kwa baadhi ya watu wa pwani msichana huruhusiwi kujipamba kama hujaolewa na hina ni moja ya mapambo nahisi kutokea hapo ndo maana ukasikia km hujaolewa huruhusiwi kupaka hina.

Siku hizi mambo yamebadilika hata mtoto wa darasa la kwanza anajua poda, wanja ndo maana imekua kawaida.

Anonymous said...

jamani, wahindi wa madhehebu ya hindu ni wajuzi sana wa hinna yaani ni mapambo yao ya asili. kwahiyo mdau wa kwanza, tuseme wahindi wanafanya makosa kupaka hinna kwa karne zote hizo? kwangu mimi hinna ni utamaduni zaidi kuliko imani ya kidini.

Anonymous said...

SHOSTI SALAMALEKO,

MWENZANGU ZAMANI KWELI HINA ILIKUWA HUPAKI LAZIMA KUWE NA OCCASSION FULANI KAMA SI HARUSI BASI HATA MINUSO MINGINE MINGINE - TENA KWA HAWA WENZETU WENYE RANGI NYEUPE ILIKUWA LAZIMA ATIE HINA NDO AONEKANE- LAKINI SASA MWENZANGU MWANAMKE HINA, TENA SHOSTI NIKUPASHE KWA SISI WENYE WAUME HINA MUHIMU MRADI RANGI IWE NDIO - MNG'ARO MNG'ARO DADA - TAFUTA HINA YAKO YA KONI ( SHOSTI SI WAJUA KONI SI YA KULA??? NIKISEMA KONI WADAU LAZIMA WATAJUA NAZUNGUMZIA NINI- JITIE VIUA SIMPLE TU SIO KIIVO KAMA MWALI WA KISUDANI MAANA WALE HUPAKWA MAUA MPAKA MGONGONI. KAMA SIO KWENYE MAPAJA TENA IKIWEZEKANA MWAMBIE MCHORAJI AKUPAKE KIDOGO KIUA NA JINA LA MUME KIUNONI - UTANIAMBIA MATOKEO YAKE.

NI MIMI,
MDAU
FATMA AMAN AU MAMA ZARINA.

Sarah Said said...

Henna ni kwa bi harusi tho siku hizi waimba rusha roho na waendaji wanapaka madai yao watu wa mwambao.. Umetaka number ya mchoraji hii 0653 468739 anaitwa Mwajuma..

Anonymous said...

Hinna ni pambo hasa kwa watu wa pwani. Na uwezi kupaka Hinna mpaka uwe umeolewa, kwa wazee wetu wa wazamani wanasema "Ukianza kupaka Hinna kabla ujaolewa siku yako harusi uwezi kupendeza" Ndiyo maana hata poda,lipstic, wanja na mapambo mengine uruhusiwi kujipamba mpaka siku ya harusi.

Mwanamke Hinna hasa ukiwa na mumeo.

RUKY said...

Kwaeli kabisa haurusiwi kupaka hina mpaka uwe umeolewa, na siku ya kwanza kupaka ni siku ya harusi
hina ni pambo kwa watu wa pwani na maana yake hasa ni kumfurahisha au kumuhamasisha mumeo. Hii maana mpka leo haijapotea kwa wanaojua maana ya hina. ila kuna hili wimbi la watu wa bara na wasiojua maana ya hina hata kwenye mahari mtu kajitia hina, kwenye kitchen party hina, ruha roho hina, wanapoteza maana halisi ya hina.

Anonymous said...

Hinna inadaiwa asili yake ni asia sana sana arabuni na india,kwa tanzania pwani. ni sunnah kupaka hinnah lkn kwa mwanammke hata mwanamme.Lkn kwa mwanamwari anaweza kupaka hinnah kwenye kucha na viganja lkn sio mikono na miguu. Na Pwani anaepaka Hinna anajulikana kabisa ameolewa, unaweza kujikuta hupati wachumba kumbe wanaume wanakuogopa wakidhania umeolewa..na sio hinna tu hata kujipodoa hairuhusiwi kama hujaolewa lkn ndo mambo ya siku hizi tena. Nadhani wengine wanafanya wafanyavyo kwa vile wanapenda/wanaona inapendeza lkn hawajui sharti zake....lkn kama hujaolewa hinnah si yako waachie kina shamim.

Anonymous said...

shamim we tafuta mtu yeyote wa pwani ya Tanga au znz(sina hakika na dar)muulize atakujibu.

Anonymous said...

habaariyako mpenzi wa blog hii.
dada zeze leo umenigusa kwa kuona hii mada ya hina.Mimi si mtaalamu sana lakini naweza kusema chochote kuhusu hina.
Kama alivyosema mchangiaji wa juu hapo kuwa hina ni pambo la mwanamke lakini pambo hili linamaana tofauti na mapambo mengine.
Kwauelewa wangu mdogo.kwanza hinna ni sunna kwa mwanamke wa kiislamu alieolewa.hii ndio maana siku ya harusi mwanamke wakiislamu hutiwa hina.
Pili:hina ni furaha ya ndoa,mwanamke kutiahina kunamaanisha mambofulani ambayo ukotayari kumfanyia bwana kwa sikuzile za hinna,mfano unampongeza kwa mafanikio yoyote aliyoyapata kimasha,karud safari ya mbali unampokea kwa hina,pia nimoja ya namna ya kukuza penzi kwaujumla ni zawadi ya bwana kwa kinamna upendavyo mwenyewe kumzawadia
kwahapa pia ningependa kuwahimiza wanaume kwamba nao wajue thamani ya hinna kwani kunawanaume ni wajinga samahani sijui kama ni ujinga au ukosefu wa mafunzo kwa hukukwetu pwani mwanamme nae hufunzwa naman ya kuichezea hina pia kiutunza KUMPA TUNZO MKE AMTILIAPO HINNA.
Ombi,jamni kinadada nasi tusifanye tena hina ndio mtego wakunasia waume wa watu tutumie ivaavyo na tusiwe sikuzote mahina miguuni kama matatoo hivi hatutapendeza ,tufanye mambo kitaalam tena kiistaarabu yawe ni suprise kwa wapenzi wetu.
Ukihitaji undanizaidi unaweza kuniuliza.

Anonymous said...

Kuna mtu kasema hapo usipake hina kama ya kisudani, nimecheka sana, mimi nina asili ya kinubi, mama yangu ni mnubi, na hina kwa kinubi ina maana kubwa. Kwa kuwa mlezi ni mama, kwa hiyo sisi tulifundishwa pia mila na desturi za kinubi.

Hina kwa kweli inapakwa watoto mpaka watu wazima, lakini kuna tofauti kubwa ya upakaji. Watoto hwapakwi maua ya aina yoyote, yaani ni plain kabisa, anapakwa hina mara nyingi usiku wa kuamkia siku ya Eid, mikono na miguu inafungwa majani ya mnyonyo, analala nayo. Hawa ni watoto wa kike na wa kiume wadogo. Watoto wa kiume wakishakuwa wa kubalehe hawapaki hina mpaka siku ya harusi. Ila watoto wa kike watapaka hiyo hina isiyo na maua mikononi na miguuni siku za sikukuu hata wakishavunga ungo.

Siku ya harusi sasa kwa mara ya kwanza kabisa binti ndio anapakwa hina yenye maua na urembo, anapakwa wanja machoni na kuwekwa urembo wa aina mbali mbali. Na siku ya bi harusi kupakwa hina huwa special, kunakuwa na mwendelezo wa shamra shamra za harusi, maana nazo zina taratibu zake, iko siku ntwaambia, basi siku ya hina kinamama wanacheza na kuimba, bi harusi akishamaliza kupakwa hina, anaachwa pale hina inakauka, sasa inabebwa sahani ya hina huku ikiwa imefunikwa vizuri, kwa nyimbo na mgoma inapelekwa kwa bwana harusi mtarajiwa. Huko na yeye anakuwa amekaa na nduguze mara nyingi wanawake wanasubiri hina kutoka kwa bi harusi. Ikifika ile hina wa kwa mke watataka kumpaka bwana harusi na wa kwa mume watatoa pesa au zawadi yoyote kuwapa ili kijana wao asisilibwe hina mkono mzima, mara nyingi huishia kupaka kwenye kidole/vidole kidogo tu kama ada. Basi hapo tena nderemo na vifijo na vigelele ndio shamra shamra za harusi hizo.

Lakini kikubwa sana ni kuwa hina ina maana kubwa sana katika mambo ya sex, na utakuta ukishakuwa nyumba kwako kwanza shurti upate ruhusa ya mume kupaka hina, sio kujipakia tu, pili sio unaenda harusini kwa watu unawapakia hina watu barabarani, tatu ukiwa mjamzito hupaki hina maana shughuli yake hutaiweza kama mume anajua maana ya hina na jinsi ya kuienjoy, inashauriwa usubiri mpaka umalize kuoga nifasi uwe tayari kumpokea mume ndio sasa unapaka hina, ndio maana unaona kinamama wengi wanapaka hina wakitoka arubaini. Hapa nazungumzia hina sio wanja ule mweusi wanaopaka watu, hina kwa maana ya hina nyekundu.

Hina pia inatumika kama dawa hasa kwa watu wazima nilikuwa nikimuona marehemu bibi yangu akipaka hina ili kuondoa maumivu ya mifupa miguuni.

Wacha hina msichana wa kinubi alikuwa haruhusiwi kuvaa pete, pete ilikuwa inaletwa siku ya posa, kwa sababu posa ya kinubi hawapeleki barua wala nini, wanapeleka pete, akikubali binti ndioo anaivaa hiyo pete yake. Kisha wa kwa mume wanapeleka jora la kushona diraa kwa mke la ndugu na jamaa zake kuvaa siku ya harusi!!