Wednesday, June 29, 2011

INASIKITISHA EEE?!!


 MO BLOG INAPENDAKUWAFAHAMISHA WADAU  NA WASOMAJI WA BLOGHII KUWA TUMESIKITISHWA NA KUHUZUNISHWA NA TABIA INAYOENDELEA YA KUHUJUMIWA NAWAPINZANI WASIOPENDA MAENDELEO YETU KWA SABABU ZAO BINAFSI.

KWA MUDA MREFU TUMEKUWA KATIKA HARAKATI NA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA TUNAWAHABARISHA,ELIMISHA NA KUJADILIANA NA WADAU MBALIMBALI WA BLOG HII BILA KUINGIA UHURU WAWENGINE WALA KUKOSOA WENGINE, KWANI MAENDELEO YA KWELI YANATOKANA NA KUJIAMINI.

KWA MANTIKI HII TUNAOWAMBA RADHI WADAU WETU  KWA KUTOKUWEPO HEWANI KWA SAA KADHAA LAKINISASA  MO BLOG IMERUDI NA ITAENDELEAKUWALETEA HABARI NA BURUDANI MBALIMBALI NANYI MSISITE KUTUSHAURI NA KUTUONGOZA KWA MAWAZO YA KUJENGA.

IKIWA NI MARA  KWAMARA TATIZO HILI LA KUPOTEA NA KUPOTEZA KAZI ZETU KUTOKEA KATIKA BLOG YETU,TUNAJIULIZA NI WAPI TUNAKOSEA AU KUHARIBU KATIKA UHABARISHAJI WETU WA HABARINA MATUKIO ,AU KUFANYA HIVI NI MAKOSA..?!!!

 KWA  KIFUPI MOBLOG  INATEMBELEWA NA WATU20,000 KWA SIKU  NA HILI LINATUPA NGUVUNA KUFAHAMU KUWA  WADAU WETUWANARIDHISHWA NA KUPENDEZWA NA  HABARI ZAKITAIFA, KIMATAIFA, BIASHARA, MICHEZO, BURUDANI NA INTERVIEWS ZA WATU MAARUFUWANAOJULIKANA NA WALE PIA WENYE VIPAJI  WASIOJULIKANA.

WADAU HILI NI KOSA…???

KWA MASIKITIKO MAKUBWA TUNAPENDA KUWATAARIFU KUWA  KAZI ZOTE ZA MWAKA HUU 2011 ZILIZOPENDWA NANYIWADAU NA NYINGINE ZIKITOKANA  NA MCHANGOWA NINYI WADAU NA WASOMAJI  ZIMEPOTEA KWALUGHA NYINGINE  (ZIMEFUTWA/ZIMEPOTEZWA)KWA SABABU AMBAZO ZINATUTIA SHAKA NA KUTUPA HISIA KUWA NI ZA  KIPINZANI.

TUSINGEPENDA KUSEMA MENGI NA WALA KUTAJANA MAJINA ILI KWAWEMA KABISA NA HEKIMA TUNAPENDA KUSISITIZA KUWA UPINZANI WA KUHARIBIANA SIMZURI NA HAUJENGI WALA KULETA MAFANIKIO KWANI MWISHO WA UBAYA NI AIBU.

HAIPENDEZI KUONGEA HAYA YOTE HAPA ILA YAKIZIDI NI AFUENI YAMOYO NI KUONGEA NA KUSEMA WAZI TUMECHOKA KUHUJUMIWA.
 ASANTE KAKA MAKWAIYAKWA MSAADA WAKO, MKUBWA MICHUZI TUNAKUSHUKURU BILA KUMSAHAU MZEE WA FULLSHANGWE NA WENGINE KWA MISAADA MBALIMBALI NA USHAURI MLIOTUPA KWETU.

WADAU WA MOBLOG TUKO PAMOJA NATUTAENDELEA KULIJENGA TAIFALETU KWA AMANI, UPENDO NA MATUMAINI.
TUNAWAPENDA, TUNAWATHAMINI, TUNAWAHESHIMU NA TUTAFANYA KAZIPAMOJA NA TUTAFIKA PALE TUNAPOKUSUDIA.

MUNGU IBARIKI MO BLOG NA WADAU WAKE WOTE.

Endelea kuperuzi MO BLOG www.mohammeddewji.com/blog

SIDHANI KAMA NI SAWA HUJUMA KAMA HIZI NAKUMBUKA NAMI BLOG YANGU ILIFUTWA MWAKA JANA...HAIPENDEZIII JAMANIII....HUJUMA HIZI WATU TUNAJIBIDIISHA NA HIZI BLOG NDO AJIRA ZETU....TUHESHIMU HII KAMA KAZI ZINGINE